Tuesday, May 20, 2014

Ahadi za Biblia

Mungu hutimiza ahadi zake. Imeandikwa katika 2Wakorintho 1:19-20 "Maana Mwana wa Mungu, Kristo Yesu aliyehubiriwa katikati yenu na sisi yaani mimi na Silwano na Timotheo hakuwa Ndiyo na siyo; bali katika yeye ni Ndiyo. Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena katika yeye ni Amin, Mungu apate kutukuzwa kwa sisi."
Mungu hazirudishi ahadi zake au kuzibadilisha. Imeandikwa katika Zaburi 89:34 "Mimi sitalihalifu agano langu, sitalibadili neno lililotoka mdomoni mwangu."
Hakuna mojawapo ya ahadi za Mungu ambazo hazijatimika. Imeandikwa katika Yoshua 23:14 "Angalieni mimi nimekwenda njia ile waendayo watu wote wa ulimwengu...... Mungu wenu katika habari zenu yote yametimia kwenu hapana neno lo lote mlilopungukiwa."
Tumeahidiwa uzima wa milele. Imeandikwa katika 1 Yohana 2:25 "Nahii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani uzima wa milele."
Mungu aweza kufanya mambo yasiyowekana. Imeandikwa katika Luka 18:27 "Akasema yasiyowezekana kwa wanadamu yawezekana kwa mungu." Tume ahidiwa moyo mpya na maisha mapya Imeandikwa Ezekieli 36:26 "Mimi nitawapa moyo mpya nami nitatia roho mpya ndani yenu nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama." Ametuahidi kutusamehe dhambi zetu. Imeandikwa katika 1Yohana 1:9 "Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote."
Ametuahidi tunda la roho. Imeandikwa katika Wagalatia 5:22-23 "Lakini tunda la roho ni upendo, furaha amani, uvumilivu, utu wema fadhili uaminifu, upole, kiasi juu ya mambo kama hayo hakuna sheria."
Ametuahi kututoa katika hofu. Imeandikwa katika Zaburi 34:4 "Nilimtafuta Bwana akanijibu, akaniponya na hofu zangu zote."
Ameahidi wokovu. Imeandikwa katika Isaya 49:25, "... Kwa maana nitateta na yeye atetaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu."
Ameahidi Roho mtakatifu Imeandikwa Luka 11:13 "Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho mtakatifu hao wamwombao?."
Atatutimizia mahitaji yetu. Imeandikwa katika Wafilipi 4:19, "Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu."
Hatatunyima lililo jema. Imeandikwa katika Zaburi 84:11 "Kwa kuwa BWANA, Mungu ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema hao waendao kwa ukamilifu."
Ametuahidi hekima. Imeandikwa katika Yakobo 1:5 "Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima na aombe dua kwa Mungu awapae wote kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa."
Mungu ametuahidi amani. Imeandikwa katika Isaya 26:3 "Utamlida yeye ambaye moyo wake umekutegemea katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini."
Mungu ametuahidi kutuepusha na majaribu. Imeandikwa katika 1Wakorintho 10:13 "Jaribu halikuwapata ninyi isipokuwa lililo kawaida ya binadamu; ila Mungu ni mwaminifu; hatawacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wakutokea ili muweze kustahimili."
Tumeahidiwa afya njema na tiba. Imo katika Biblia, Yeremia 30:17 "Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema BWANA..."
Mungu ameahidi kutulinda na hatari na ajali. Imeandikwa katika Zaburi 91:10 "Mabaya hayatakupata wewe, wala tauni haitaikaribia hema yako."
Biblia yatuahidi ya kwamba waliokufa watafufuka katika ufufuo. Imeandikwa katika Yohana 5:28-29 "Msistaajabie maneno hayo kwa maana saa yaja ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale walio fanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wao walio tenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu."
Yesu ameahidi ya kwamba atarudi tena. Imeandikwa katika Yohana 14:2-3 "Nyumbani mwa Baba yangu kuna makao mengi; kama sivyo ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaanadalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu ili nilipo nanyi muwepo."
Ameahidi kukomesha vifo, maumivu na dhiki. Imeandikwa katika Ufunuo 21:4 "Naye atafuta kila chozi katika macho yao wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita."

Monday, May 19, 2014

IBADA YA JUMAPILI 18.5.2014

Ibada ya jumapili 18.5.2014 iliongozwa na Mtumishi wa Mungu Timothy Mwansasu
Ujumbe katika ibada hiyo ulikuwa ni MAMBO YOTE UNAYOYAOGOPA YAONDOKE KWAKO
Neno lilitoka katika kitabu cha Samweli 1
1samweli 7:1-12
hapa tunasoma habari za mfalme Hezekia na kupewa taarifa juu ya kifo chake na Nabii wa Mungu Samweli.
Mtumishi wa Mungu Mwansasu alisema wakristo wengi wa leo si kama mfalme Hezekia,alipopata habari kutoka kwa Nabii wa Mungu kuwa atakufa,yeye hakutaka kusema na Nabii,kwa kuwa alimjua Mungu.
Alichokifanya aligeukia ukutani akalia sana na ndipo Mungu akasikia kilio chake na kumuongezea miaka kumi na tano zaidi ya kuishi.
Mtumishi Mwansasu alisema kuna jambo gani ambalo ni gumu sana mbele yako.Lipeleke kwa Mungu na hata kama lilikuwa likioneka gumu kiasi gani mbele yake hakuna gumu.
Alisisitiza kusanyiko kuwa watu wa Maombi ,maana kwa maombi pekee unaweza kuyashinda magumu

Zifuatazo ni baadhi ya picha kwenye ibada hiyo

Mtumishi wa Mungu Akili akiongoza Maombi ya kufungua Ibada

KIPINDI CHA SIFA
Mtumishi Timothy Mwansasu akiongoza kusanyiko kuimba nyimbo za TENZI ZA ROHONI



Kusanyiko

Mtumishi wa Mungu Joseph Sambai akimwimbia Mungu

Dada Teddy naye aliimba wakati wa kipindi cha sifa

Huyu ni Mtumishi wa Mungu Davies 
Kwaya ya kanisa 



Mama Mchungaji akisema na kusanyiko

WAKATI WA NENO LA MUNGU

Mtumishi wa Mungu Mwansasu akifundisha neno la mungu kwenye Ibada hiyo



WAKATI WA MAOMBEZI















Thursday, May 15, 2014

IBADA YA JUMAPILI 11.5.2014 PAMOJA NA IBADA YA SIFA ILIYOFANYIKA JIONI

Mungu bado ni mwema katikati ya Paradise,Pamoja na kazi kubwa ya kumjengea Mungu Hekalu .
Lakini kusudi la la kufanya Ibada za sifa na Kuabudu litabakia pale pale,Tar 11.5.2014 Kulikuwa na Ibada ya kusifu na kuabudu ,Hizi ni baadhi ya picha na ibada ya Asubuhi pamoja na Ibada ya Kusifu na Kuabudu inayofanyika  kila jumapili ya mwanzo wa mwezi.

IBADA YA ASUBUHI:

Kiongozi wa Sifa wa siku hiyo Mtumishi wa Mungu Timothy Mwansasu akiongoza kusanyiko kuimba nyimbo za Tenzi za rohoni katika kipingi cha sifa cha ibada ya Asubuhi

Mtumishi wa Mungu Ruben Akiongoza Kusanyiko katika kusifu

Wapiga vyombo watumishi wa Mungu Eddy na Enosh wakitumika

Kwaya ya kanisa Paradise Choir

Praise Team


Praise Team



BAADA YA IBADA WAMAMA WA PARADISE WALIMTEGEMEZA MCHUNGAJI
Wamama wakiwa na Saadaka zao tayari kuzitoa kwa Mtumishi wa Mungu












IBADA YA SIFA JIONI



Hata Mchungaji pia alisimama na kumsifu Mungu




Ilifika wakati watu walishindwa kukaa kwenye viti na waliinuka na kumchezea Mungu wao

Praise Team

Kiongozi wa Ibada ya Kusifu na Kuabudu Mama Mchungaji akiongea

Mtumishi wa Mungu Irene Mwakajila akimuimbia Mungu kwenye ibada hiyo ya Sifa 


Huyu ni Mtumishi wa Mungu Majaliwa akiimba "Kwa msaada wa Roho tunashinda yote ya Dunia"