Monday, August 11, 2014

BARAKA ZETU ZIPO KATIKA NENO.



Mchungaji Lugano Mwakisole

BARAKA  ZETU  ZIPO  KATIKA  NENO.
MATHAYO  4 :4  "mtu hataishi kwa mkate tu  bali  kwakila  neno litokalo  katika  kinywa  cha Mungu"
Wapendwa wasomaji napenda tushirikishane jambo kuu sana lina lohusu baraka.kila mtu anapenda baraka lakini ni muhimu kufahamu msingi wa baraka zetu tuliookoka unapatikana wapi,na wenzetu au mababa zetu wa Imani katika biblia walipata baraka kupitia nini?soma zaidi upate kuelewa.

KUNA TOFAUTI YA KUFANIKIWA NA KUBARIKIWA.
Mafanikio ni matokeo ya mwilini bali baraka zinaanza rohoni nakuonekana mwilini.Mtu aliyefanikiwa anaweza akawa na pesa,magari,majumba ya kifahari(matokeo ya nje) lakini akawa hana amani,furaha ya ki Mungu na upendo wa ki Mungu.pia ni mtu anayeishi kwa masharti mazito,na hofu tele juu ya utajiri wake,hii tena si baraka bali ni mafanikio tu,baraka ni matokeo ya rohoni kwanza inayobeba furaha,amani na upendo wa ki Mungu.Baraka inaanza rohoni kwa vitu hivyo nilivyovitaja(upendo,furaha na amani ya kiMungu) ndipo inadhihirika mwilini kama matokeo ya utajiri wa fedha,nyumba,magari nk.Mtu akipata vitu vya mwilini akakosa amani na vitu hivyo au furaha ya Mungu anakuwa ni mtu wa huzuni,anakosa upendo na ndugu zake au marafiki,mara nyingine anakuwa na ukali usio na sababu, msongo wa mawazo japo ana kila kitu.Anapungukiwa na baraka au vitu vya ndani (rohoni)vitakavyomfurahisha kwanza bali vinavyoonekana na matokeo yake yanakuwa ni mabaya.Anaweza kuacha vyote na ukashangaa analala kwa mganga wa kienyeji au mpunga pepo,katika mazingira machafu yasiyoendana na yeye.tatizo alidhani baraka zinaanzia mwilini kumbe baraka zinaanza rohoni na kumalizikia mwilini.maandiko yanasema"utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki zake na mengine tutazidishiwa"Haki zinazosemwa hapo ndio hizo furaha amani pendo za kiMungu na mengine tunayozidishiwa ni utajiri tunaouona kama fedha, magari,majumba n.k Na baraka zetu zinajengwa na neno la Mungu na huu ndiyo msingi wetu.

 Maisha yetu,kuishi kwetu,kula  yetu,vaa  yetu  na  baraka  zetu  zimebebwa katika neno.  Na  hii  ndio  maana ya kusema tunaishi  kupitia  neno  analosema Mungu.(math 4:4).Pia  andiko  la EBRANIA 10 : 38 linasema "mwenye haki   wa mungu ataishi kwa imani" inapoongelewa imani  inamaanisha  kusikia neno la kristo ,(WARUMI 10 :17)  Hapo tunapata picha zaidi   kuwa maisha yetu  yote  na  mafanikio yamebebwa  na neno la Mungu:

Neno humjenga mtu katika imani  na  imani inasababisha  baraka zote za kimwili  na kiroho.watu wengi wanapenda kubarikwa lakini  hawataki kuishi kwa neno,kulisoma neno,au kusikia kupitia watumishi wa Mungu.Hawaendi kanisani kukutana na mtoa baraka kwa kisingizio wana kazi nyingi. Ni  vigumu watu  hawa kupata baraka za kiMungu.Baraka huja kupitia neno  la Mungu, unapolisikia na kulitendea  kazi ,  na Baraka inaanzia  rohoni  ndipo hudhihirika mwilini .Yohana aliandika waraka wake  " 3YOHANA 1 :2 mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na  Afya njema kama vile roho yako  ifanikiwavyo" akiwa anamanisha baraka zote zinaanza rohoni  ndipo inadhihirika mwilini

MIFANO YA WATU WALIOBARIKIWA KUPITIA NENO LA MUNGU
 1. Ibrahimu baba wa imani(MWANZO 12:1-3)
Ibrahimu aliambiwa neno na Mungu  atoke aende katika nchi  ambayo aliandaliwa baraka tele.
Baraka zilianza pale tu Ibrahimu alipotii neno au agizo na akatekeleza.mstari wa 4 ibrahim alitekeleza na alipotoka baraka zilimfuata kama neno liliivyomwambia.japo alipitia mitihani mingi lakini ushindi wa mwisho ulikuwa mkuu sana na matokeo yake ni makubwa,Tunaona matokeo ya taifa la israel ni kutokana na kutii kwa ibrahim.ishi kwa neno na kutii kama Ibrahim utaziona baraka kwako na familia yako na hata kizazi chako chote.   
2 NABII ELIYA:  WAFALME 17 :1-16
 Hapo tunaona maisha alioishi Eliya baada ya kutokea njaa iliyosababishwa na maombi yake mwenyewe. Baada ya kuzuia mvua kulikuwa na ukame   na njaa kubwa katika  mji wa israeli  wakati huo mgumu  watu wengi  walisumbuka  sana kutafuta chakula  lakini Eliya  kwake maisha hayakuwa magumu sababu  yeye aliishi kwa neno la Mungu.  
 Ukisoma mstari  2-7  Neno lilimjia Eliya  aende katika kijito cha kerithi. Alipotii  kwenda huko  Mungu alikuwa amemwandalia kunguru wamlishe  katika kijito  hicho na kunywa maji hayo.   wakati huo mgumu , Eliya haukumsumbua  kwasababu  yeye alitii neno la Bwana na aliweza kuishi.Hali ngumu za maisha  au kukosa pesa si sababu ya kukata tamaa kwani tukiamini neno lake,Mungu atafungua njia juu yetu.kumbuka neno linasema "dunia na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana,ZABURI 24:1.Pia anatupa ahadi kuwa tukimwomba yeye atatupa kwa kuwa na sisi ni watoto wake.(MATH 7:7-11)
Mstari 8:16  katika 1wafalme 17 tumeona kijito  kilikauka kutokana  na hali ya ukame, lakini  hilo  halikumtisha  Eliya  bali alisikiliza maelekezo ya neno.  Ndipo neno likamwongoza kwenda kwa mwanamke mjane wa serepta na akafanya muujiza kupitia mafuta kidogo  katika chupa na unga kidogo. Na muujiza mkubwa ukafanyika wakaishi.
   Eliya hakutishwa na mabadiliko ya hali ya hewa bali aliamini neno kuwa litamfanya aishi . Je  ni kitu gani kinakufanya uwe na hofu ya maisha, je kukosa kazi, mabadiliko ya uchumi, au kukataliwa na ndugu au jamaa.? Vyote hivyo haviwezi  kuzuia baraka zetu sababu sisi hatuishi kwa bahati(hatubahatishi  maisha)  bali maisha yetu yanaongozwa na neno (MATHAYO 4:4).Watu wasiookoka wanaishi kwa bahati na ndio maana wanaishi kwa wasiwasi na wengine husema "bahati hairudi mara mbili"sababu wanabahatisha wanakuwa na hofu wakifilisika utakuwa ndio mwisho wao.Sisi tuliookoka tunaishi kwa neno au maongozi ya neno na baraka zetu ni nyingi hata zikizuiliwa na shetani au watu wenye hila sehemu fulani,iwe kufukuzwa kazi,kudhurumiwa,kutendewa mabaya na  watu  tuliowaamini lakini wakageuka,bado Mungu atafungua kwa njia nyingine. Sisi ni wabarikiwa na ni kipawa tulichopewa kama biblia isemavyo"kipawa ni kito cha thamani na kila kigeukapo hufanikiwa,)Maana ya kila kigeukapo inamaanisha kila uendapo na kila ufanyacho utafanikiwa.Shetani japo alijaribu kugusa maisha ya Ayubu kwa magonjwa,kuuwa watoto wake na mifugo na mali zake kufilisiiwa,bado alimtegemea Mungu na matokeo ya mwisho yalikuwa mazuri kuliko mwanzo na alipata utajiri mwingi kuliko mwanzo.Hata kama shetani alichezea uchumi wako na ukakata tamaa,nakutia moyo kuwa baraka yako bado ipo si za kubahatisha,Yesu atakubariki kwani anazo baraka nyingi.Pia baraka zetu zinatufuata popote tunapoenda kama neno lisemavyo " hakika wema na fadhiri  zitatufuata  siku zote za maisha yetu, ZABUR 23:6"
Pia baraka zetu anayetoa ni Mungu na ndie anatupa nguvu za kupata utajiri(  KUMB 8:17:18)  Wala si uwezo wetu hivyo tumtegemee yeye  ambae ndiye neno  (YOHAN 1:1)  Ili atupe mahitaji yetu,

 Vitu vyote vipo chini yake na anatoa kwakila mtu anaye mcha na kumtii( 1MAMB NYKT 29:12).

Ushauri wangu kwako mpe Yesu maisha yako utapata baraka za Bwana ambazo zinajumuishwa na upendo,furaha,na amani kisha utajiri wa fedha,mifugo,mashamba,majumba,magari n.k Bwana atatuzidishia na baraka ya Mungu inaenda hatua kwa hatua,yapasa uwe mvumilivu kama baba yetu Ibrahim aliyepita wakati mgumu lakini mwisho wake ulikuwa mzuri.Usitake utajiri kwa haraka dunia itakupoteza.wengi tunawaona walitaka utajiri kwa haraka lakini wamekufa mapema tena kwa vifo vya kuhuzunisha na pesa na utajiri wao hawakuufaidi bali wamefaidika wengine.Baraka ya Mungu hutajirisha na haichangamani na majuto.Mungu awabariki.

Kwa Msaada Zaidi
Waweza kuwasiliana nami
0688387834
luggymakky@gmail.com

No comments:

Post a Comment

Andika maoni yako hapa

Note: Only a member of this blog may post a comment.