Thursday, September 4, 2014

KUWA RAFIKI WA KARIBU WA YESU-Somo linaendelea:Mch Lugano Mwakisole

MCHUNGAJI LUGANO MWAKISOLE



KUWA RAFIKI WA KARIBU WA YESU


Mungu ni mwema ametukutanisha tena katika Blog hii ili kujifunza neno lake,
Leo tutaendelea kujifunza HATUA ZA KUWA RAFIKI WA KARIBU WA YESU,
Juma liliopita tulijifunza hatua nne na leo tutaendelea na hatuna nyingine,
Kama hukusoma hatua ya kwanza mpaka ya tatu bofya hapa

HATUA ZA KUWA RAFIKI WA KARIBU WA YESU
4.Hatua ya nne ni kushiriki mateso pamoja naye(1Petro4:12-16)
-Unapokuwa rafiki wa Yesu hautapata raha tu bali na mateso pia.Yesu anaruhusu mateso na majaribu yakupate ili kupima urafiki wenu upo imara au la.Kila mtu aliitwa na Yesu na kuokoka kwa njia tofauti.Wengine waliitwa kwa kuponywa magonjwa mbalimbali,wengine waliombewa wakapata ajira au kupandishwa vyeo makazini ndipo walipoamua kuokoka,wengine walipoombewa biashara zao zikafanikiwa wakachukua uamuzi wa kuokoka.Vyote hivi vilikuwa vivutio vya wokovu kwa upande mmoja,Na kila mtu alipopata baraka hizi alishuuhudia kwa ujasiri na aliuona upendo wa Yesu ulivyo mkuu na wa ajabu.Lakini kuna kiwango kingine cha kuuona upendo wa Yesu katika majaribu,dhiki,udhia,msiba,magonjwa,kukosa kazi,kukosa hata familia kwa ajili ya Yesu. Hapa anatafutwa mwanafunzi kwelikweli au rafiki wa Yesu atakayeshinda mapito yote na kustahimili.
Ona Mifano hii:-
1-Wanafunzi wawili walimwomba Yesu mmoja akae kulia kwake na mwingine kushoto katika ufalme wake.(Mathayo 20:20)Yesu aliwauliza nao kama kweli wataweza kukinywea kikombe chake? akimaanisha wanaweza kushiriki mateso pamoja naye? Kutaka kuwa karibu naye ni kukubali kushiriki mateso naye.Ni wengi hupenda kuwa karibu naye lakini hawawezi kushiriki Mateso pamoja naye.Baada ya muda kupita Yesu aliwachukua wale wanafunzi ili kuwapima kama kweli wanaweza kukinywea kikombe pamoja naye lakini wakati wa kuomba wanamwacha Yesu peke yake,wanalala.(Math 26:37).Ili uwe rafiki wa karibu wa Yesu ni lazima ukubali kushiriki mateso naye.
2-kuna sehemu nyingine naipenda wakati Yesu amegawa mikate kulisha makutano,walikula watu elfu tano hao ni wanaume tu,ukichanganya na wanawake na watoto ni umati mkubwa sana wa watu pengine ingekuwa vigumu hata kuhesabu.(Yohana6:1-11),lakini siku zilipofuata Yesu anabadilisha chakula kawaambia wale mwili wake na wanywe damu yake,(Yohana 6:26-58) hapa watu wote wakakimbia walibaki waume kumi na mbili tu.Lilikuwa fumbo zito akimaanisha kwake hakuna mikate tu yaani miujiza tu au raha tu kuna kushiriki mwili na damu ikimaanisha kushiriki mateso pamoja naye,na hapa yanamaanisha mateso ya msalaba(Mathayo 26:28).Msalaba ni kukubali kuteseka kwa ajili ya Yesu,kukubali hata kukosa mume au mke au kufukuzwa na wazazi sababu ya kuokoka.(Mathayo 10:34-39)msalaba ni kujikana na kumfuata Yesu inabidi ujitoe kwa dhati.Kubali hata kupoteza utu wako,familia,mume au mke kwa ajili ya Yesu.
-pia ni lazima ukubali kujikana na kubeba msalaba(Mathayo16:24-27).msalaba ni mateso lakini ndiyo ushindi wetu,msalaba ni aibu,kubali aibu kwa ajili ya Kristo.Kubali kunenwa kuwa umechanganyikiwa,kuacha starehe,anasa,dhambi zote hata kama zinavutia kwa ajili ya kristo.unaweza ukaona wenzako kazini wanaiba kwa kuchengesha mahesabu na unaona wanafanikiwa kuwa na nyumba nzuri,magari n.k.wewe usifuatishe acha,jikane,huko ndiko kubeba msalaba.
-Naomba nikukumbushe tenzi za Rohoni wimbo usemao" Bwana u sehemu yangu "kuna mahali mtunzi ameandika"mahali hapa sikutaka niheshimiwe na yanikute mateso sawa sawa na wewe."na chorus yake inasema pamoja na wewe ukimaanisha ushirika na Yesu katika mateso pia.ILI UWE RAFIKI WA YESU KUBALI KUSHIRIKI MATESO PAMOJA NAYE.

5.Hatua ya tano ni uaminifu.(1Kor 4:1-2),Rafiki wa Yesu anajua siri za Mungu nyingi anatakiwa kuwa mwaminifu sana,neno hili kuna maneno mawili ambayo imani na kamili.ili mtu awe mwaminifu lazima awe na imani kamili au imani iliyojitosheleza(faithfull).Na imani kamili ndiyo inatimizwa na kutii kila amri ya kwenye biblia.Kuna siri nyingi utapewa kama rafiki yake na si zote za kusema kwa wakati huo,nyingine unaweza kuambiwa uombe wewe mwenyewe,na nyingine utekeleze kwa matendo,nyingine anaweza kukwambia kama rafiki yake mpendwa lakini hazina utekelezaji japo kakushirikisha,zipo katika mapenzi yake hauwezi badilisha.(Zaburi25:14)

Mfano:
Mungu anaweza kukuambia habari ya mtu kuwa atamchukua au kifo kitampata.hapo pana mambo ya kuzingatia.Je Mungu ameruhusu au ni roho ya mauti.kama roho ya mauti unaweza kukemea lakini kama ni mapenzi yake unapaswa kushukuru.lakini pia inaweza ikawa mapenzi yake lakini ukamsihi asimchukue kwa kupeleka hoja zenye nguvu kwake na kumsihi kama ombi lakini si amri.Yesu aliomba baba ikiwezekana kikombe kiniepuke.sehemu hiyo akutumia mamlaka sababu ni sehemu ambayo ilikuwa katika mamlaka ya Mungu.ni lazima uelewe maombi ya kusihi mapenzi ya Mungu na sehemu ya kutumia mamlaka.Sisi tumepewa kumtii Kristo pia tumepewa kumpinga shetani(Yakobo 4:7)Tukiomba vibaya bila kuelewa hatupati majibu.Mtu anayefikia hatua ya kuwa mwaminifu ataambiwa siri na Mungu hata za mambo yanayotokea mbele kama misiba,baraka,njaa,vita n,k,mengine ni ya kusema na mengine si ya kusema inategemea na maongozi ya Roho Mtakatifu.Mtu mropokaji sana ,asiyetulia,hawezi kupewa siri nyingi.anatafutwa MWAMINIFU ndiye anastahili kuambiwa mambo ya Bwana na atasema kwa maongozi ya Roho tu.Utulivu wa Yohana ulimsaidia kuandika kitabu cha ufunuo chenye siri kubwa juu ya siku za mwisho.Mungu alimteua Musa kuongea naye na kisha kupeleka maagizo kwa Israel.Musa alijua siri za Mungu kutokana na uaminifu wake.maono mengine Mungu anaweza kukupa lakini si ya sasa,ukikurupuka kusema yanaweza kukuletea matatizo.Manabii walipewa mambo ya miaka mingi ijayo na mpaka wanakufa hawakuyaona.wengine wakiambiwa upenda kusema haraka ili wajikweze kuwa wenyewe ni manabii wa kweli.Watu kama hao ni rahisi kushuswa au kutopewa tena.

Mungu awabariki somo litaendelea ili kuzifahamu faida za kuwa rafiki wa Yesu.

Video ya somo hili:https://www.youtube.com/watch?v=qoBJ4EJZmMU

Mchungaji:Lugano Mwakisole


EAGT Paradise Mbagala Zakhem

No comments:

Post a Comment

Andika maoni yako hapa

Note: Only a member of this blog may post a comment.