Ilikuwa ni neema kwa kanisa la Eagt Paradise kwa kuwa na semina ambayo ilianza tar 19.2.2014 na kumalizika tar 23.2.2014 ambayo iliendeshwa na Mama yake Frola Mbasha.
Katika kumalizia kwake Mtumishi wa Mungu alisisitiza sana kwamba sisi ni wa thamani sana mbele ya Mungu.
Alisema wakati ule wa utawala wa mfalme Nebkadneza,vijana waliomjua Mungu yaani Meshaki,Shedraki na Abednego wao walijua uthamani wao na Mungu wao.
Angalia baadhi ya picha kwenye ibada hiyo
 |
Mtumishi wa Mungu Reuben akimsifu Mungu |
 |
Dada Irene naye ilikuwa ni zamu yake kusimama mbele za Mungu na kumwimbia |
 |
Pichani ni kwaya ya kanisa ikimsifu Mungu |
 |
Huyu ni mtumishi wa Mungu Mwangosi alitutembelea naye akapata nafasi na ujumbe wa nyimbo yake ulikuwa ni ule ule kuwa wewe ni wa thamani sana mbele za Mungu |
 |
Mchungaji kiongozi Lugano akisema na kanisa |
 |
Ulifika wakati wa kumkaribisha muhudumu,pichani Mama Mchungaji akimwinua Mumishi wa Mungu Mama Mbasha |
 |
Karibu mama utupe Chakula cha Roho ni kama maneno ambayo anayasema mbele ya mtumishi wa Mungu Mama Mbasha madhabahuni |
 |
Wewe ni wa thamani sana mbele za Mungu |
 |
wakati wa maombezi |
 |
Wamama wa Eagt Paradise wakipeleka zawadi kwa mtumishi wa Mungu Mama Mbasha |
 |
Mwenyekiti wa wamama wa Eagt Paradise Judy Mecky akimshukuru Mtumishi wa Mungu kwa kipindi chote alichokuwa nasi |
 |
Mtumishi wa Mungu akuwashukuru wamama na kanisa kwa ujumla |
No comments:
Post a Comment
Andika maoni yako hapa
Note: Only a member of this blog may post a comment.