Nawasalimu kwa jina kuu la Yesu wasomaji wote wa Blog hii,
napenda kushiriki nanyi kile kilichofundishwa jana katika ibada,Tulipata mgeni kutoka Turiani Morogoro,Mtumishi wa Mungu Joshua Malundo yupo nasi kwa wiki ya pili sasa.
Anaendelea kutuletea yale mungu aliyompa kusema nasi.
Mungu alisema nasi juu ya UMUHIMU WA MABADILIKO,
Msingi wa somo hili ulitoka katika maandiko ya Mungu katika kitabu cha 1Samwel 10:1-7,
Kuna umuhimu mkubwa sana wa sisi kama watu wa Mungu kubadlika na hilo ndilo Mungu anatamani sana kuliona kutoka kwetu.Hata yeye alipotuokoa alitubadilisha kutoka kwenye utu wa kale na kutuvika utu upya.Lakini katika mabadiliko yapo yaliyo mbadiliko sahihi na ambayo si sahihi.
Badiliko linalotka kwa Mungu huwa ni sahihi sikuzote.Hitaji badiliko sahihi katika kila eneo la maisha yako.
Sehemu za picha katika ibada hiyo
 |
kipindi cha Sifa |
 |
Sehemu ya kusanyiko |
 |
Mtumishi wa Mungu akitoa shukrani kwa kupata mtoto salama |
 |
Mtumishi wa Mungu akimshukuru Mungu baada ya maombi yaliyofanyika kanisani hapa kwa wiki moja,Mungu ameanza kufungua njia katika kazi za mikono yake |
 |
Mwenyekiti msaidizi wa ujenzi wa Hekalu la Mungu,naye alimshukuru Mungu kwa kumponya mguu wake uliovunjika wiki mbili zilizopita |
 |
Baraka kutoka kwa Mchungaji |
 |
Kwa Mungu wote ni vijana akimwimbia Mungu |
 |
Mtumishi wa Mungu Teddy Komba |
 |
Praise Team |
 |
Tutamsifu Mungu kwa kila hali |
 |
Mwinjilisti Joshua Malundo akifundisha |
 |
Wakati wa Maombezi |
 |
Darasa la watoto |
No comments:
Post a Comment
Andika maoni yako hapa
Note: Only a member of this blog may post a comment.