Monday, November 25, 2013

IBADA YA JUMAPILI 24.08.2013

Biblia ina sema tusiache kukutanika,Jumapili Tar 24.13.2013 Katika kanisa la EAGT Paradise Praise Centre ilifanyika ibada ya kumwinua na kumtuka Mungu.
Ibada iliongozwa na Mchungaji Kiongozi Lugano Mwakisole na ikiwa ni muendelezo wa ibada za Kufanywa Upya.

Tunakuletea matukio ya ibada hiyo katika picha

1.KIPINDI CHA SIFA


Kiongozi wa Sifa katika ibada hiyo Mtumishi wa Mungu Reuben Akiongoza kusanyiko kumsifi Mungu

Wapiga vyombo wakimtukuza Mungu wakati wa kipindi cha Sifa






Mtumishi wa Mungu Anthony ambaye ni mgeni kutoka Arusha alitembelea EAGT Paradise Praise Centre naye alipata nafasi kumwimbia Mungu wetu


Mama huyu hata katika uzee wake bado anatumikia Mungu na yeye anasema Kwa Mungu hakuna Mzee

Kwaya ya Kanisa nayo haikuwa nyuma ili mradi Mungu ainuliwe

Watumishi wa Mungu wakimtumikia Mungu

2.KIPINDI CHA KUABUDU
Kilifika kipindi cha Kumwabudu Mungu wetu

Yafaa kumwabudu Mungu maana hakuna kama yeye

3.MAHUBIRI

Mchungaji Kiongozi Lugano Mwakisole akileta kusudi la Mungu mbele ya watumwa wa Mungu




HATA WEWE UNAKARIBISHWA KWENYE IBADA ZETU ZINAZOANZA KILA JUMAPILI SAA 1.OO ASUBUHI



Friday, November 22, 2013

MKUTANO WA INJILI MBAGALA KICHEMCHEM 16.11.2013

Ni agizo la Bwana Yesu kuihubiri injili na kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi wa Yesu.
Kanisa la Eagt Paradise Praise Centre siku ya Jumamosi Tar.16.11.2013 liliendesha mkutano wa Injili Eneo la Mbagala Kichemchem.
Katika Mkutano huo Mungu alionekana na watu wengi wenye vifungo mbalimbali bwana Yesu aliwafungua 






Tunakuletea baadhi ya Picha za matukio katika mkutano huo


Kwaya ya Kanisa la Eagt Praise Centre wakihudumu kwenye mkutano


Kwaya ya wamama wa Eagt Paradise Praise Centre wakihudumu 


Kwa Mungu hakuna mzee,ni mama mtu mzima ambaye hata kwenye uzee wake bado anamtumikia Mungu akihudumu kwa njia ya uimbaji kwenye mkutano huo

Mtumishi wa Mungu Davies akihudumu kwa njia ya uimbaji

Ukiwa na Yesu kweli raha,hapa mtumishi wa Mungu Mwinjilisti Paul akicheza 

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Eagt Paradise Praise Centre,Mch.Lugano Mwakisole akiangalia watenda kazi kwenye mkutano huo uliofanyika Kichemchem Mbagala


Mwinjilisti Timothy Mwansasu akihubiri katika mkutano huo


Na zamu ya Mwinjilisti Isaya ilifika na yeye alileta lile kusudi la Mungu



Ni baadhi ya watu waliohudhuria mkutano huo