Thursday, August 29, 2013

BREAKING NEWS: ASKOFU MOSES KULOLA AFARIKI DUNIA




Taarifa zimeenea  hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia muda mfupi uluopita.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika ambazo tumezipata kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.

Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.

Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.



Gospel Kitaa itaendelea kukufahamisha kwa kadri ambavyo taarifa zitakuwa zikitufikia.Kufahamu historia ya maisha ya Hayati Askofu Dr. Moses Kulola .

BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe.


Source:Gospel Kitaa

Monday, August 26, 2013

ANGALIA PICHA ZA MKUTANO WA REINARD BONNKE VIWANJA VYA TAIFA

Angalia baadhi ya picha za mkutano mkubwa wa injili ulioandaliwa na huduma ya mwinjilisti wa kimataifa Reinhard Bonnke akiwakilishwa na kijana wake katika huduma Daniel Kolenda, mkutano ambao unafanyika katika uwanja wa nje wa taifa jijini Dar es salaam. ukishirikisha watumishi kutoka makanisa mbalimbali.