Saturday, October 5, 2019

Soma Hiyoo! kutoka kwa Rev.Mathayo Henry


Image may contain: 1 person, hat

Mzee mmoja kabla hajafa, alimpa kijana wake saa kongwe kama kumbukumbu maishani. Akamwambia," huu ni urithi kutoka kwa babu yako.. Hii saa Ina umri wa zaidi ya miaka 200. Ili ujue thamani yake, nenda kaulize kwenye duka la saa mwisho wa mtaa. Waambie unataka kuiuza, waulize watakupa sh ngapi? ."

Kijana akarudi kwa babake na kumwambia jamaa wa dukani wametaka kulipa Shilingi 5000, kwa sababu saa ni ya zamani Sana.. Yaani imechakaa.."

Mzee akatabasamu Kisha akamwambia kijana wake, " nenda kwa muuza kahawa ukamsikilize pia."

Kijana akaenda kwa muuza kahawa. Muuza kahawa nae akaja na ofa ya sh 5000 pia, akidai saa ni ya zamani.. Kijana akampelekea jibu mzee wake. Mzee akatabasamu na kumwambia mwanae, " Nenda kwenye duka la kumbukumbu za vitu vya kale, Kisha uwaonyeshe hiyo saa.. Lile duka la mzungu pale posta.."

Kijana akarudi kwa babake akiwa na furaha.., " Baba, mzungu amesema atalipa milioni 8 kwa hii saa kongwe hadi nimeshangaa Wallahi. Sijaamini.. "

Mzee akasema," Nilitaka ufahamu kuwa pahala sahihi au watu sahihi ndio watakaofahamu thamani yako mwanangu. Daima usijipendekeze kwa watu wasiojua thamani yako. Jisogeze kwa watu wanaoijua thamani yako.. "

Anaejua thamani yako, atakuthamini.. Usijilazimishe kukaa na wasiokuthamini.. Usijilazimishe kuishi usipopendwa.."

Tambua thamani yako ndugu yangu.. SHIRIKIANA NA WATU WANAOJUA THAMANI YAKO!! MUNGU AKUINUE KATIKA YOTE.

Thursday, September 4, 2014

KUWA RAFIKI WA KARIBU WA YESU-Somo linaendelea:Mch Lugano Mwakisole

MCHUNGAJI LUGANO MWAKISOLE



KUWA RAFIKI WA KARIBU WA YESU


Mungu ni mwema ametukutanisha tena katika Blog hii ili kujifunza neno lake,
Leo tutaendelea kujifunza HATUA ZA KUWA RAFIKI WA KARIBU WA YESU,
Juma liliopita tulijifunza hatua nne na leo tutaendelea na hatuna nyingine,
Kama hukusoma hatua ya kwanza mpaka ya tatu bofya hapa

HATUA ZA KUWA RAFIKI WA KARIBU WA YESU
4.Hatua ya nne ni kushiriki mateso pamoja naye(1Petro4:12-16)
-Unapokuwa rafiki wa Yesu hautapata raha tu bali na mateso pia.Yesu anaruhusu mateso na majaribu yakupate ili kupima urafiki wenu upo imara au la.Kila mtu aliitwa na Yesu na kuokoka kwa njia tofauti.Wengine waliitwa kwa kuponywa magonjwa mbalimbali,wengine waliombewa wakapata ajira au kupandishwa vyeo makazini ndipo walipoamua kuokoka,wengine walipoombewa biashara zao zikafanikiwa wakachukua uamuzi wa kuokoka.Vyote hivi vilikuwa vivutio vya wokovu kwa upande mmoja,Na kila mtu alipopata baraka hizi alishuuhudia kwa ujasiri na aliuona upendo wa Yesu ulivyo mkuu na wa ajabu.Lakini kuna kiwango kingine cha kuuona upendo wa Yesu katika majaribu,dhiki,udhia,msiba,magonjwa,kukosa kazi,kukosa hata familia kwa ajili ya Yesu. Hapa anatafutwa mwanafunzi kwelikweli au rafiki wa Yesu atakayeshinda mapito yote na kustahimili.
Ona Mifano hii:-
1-Wanafunzi wawili walimwomba Yesu mmoja akae kulia kwake na mwingine kushoto katika ufalme wake.(Mathayo 20:20)Yesu aliwauliza nao kama kweli wataweza kukinywea kikombe chake? akimaanisha wanaweza kushiriki mateso pamoja naye? Kutaka kuwa karibu naye ni kukubali kushiriki mateso naye.Ni wengi hupenda kuwa karibu naye lakini hawawezi kushiriki Mateso pamoja naye.Baada ya muda kupita Yesu aliwachukua wale wanafunzi ili kuwapima kama kweli wanaweza kukinywea kikombe pamoja naye lakini wakati wa kuomba wanamwacha Yesu peke yake,wanalala.(Math 26:37).Ili uwe rafiki wa karibu wa Yesu ni lazima ukubali kushiriki mateso naye.
2-kuna sehemu nyingine naipenda wakati Yesu amegawa mikate kulisha makutano,walikula watu elfu tano hao ni wanaume tu,ukichanganya na wanawake na watoto ni umati mkubwa sana wa watu pengine ingekuwa vigumu hata kuhesabu.(Yohana6:1-11),lakini siku zilipofuata Yesu anabadilisha chakula kawaambia wale mwili wake na wanywe damu yake,(Yohana 6:26-58) hapa watu wote wakakimbia walibaki waume kumi na mbili tu.Lilikuwa fumbo zito akimaanisha kwake hakuna mikate tu yaani miujiza tu au raha tu kuna kushiriki mwili na damu ikimaanisha kushiriki mateso pamoja naye,na hapa yanamaanisha mateso ya msalaba(Mathayo 26:28).Msalaba ni kukubali kuteseka kwa ajili ya Yesu,kukubali hata kukosa mume au mke au kufukuzwa na wazazi sababu ya kuokoka.(Mathayo 10:34-39)msalaba ni kujikana na kumfuata Yesu inabidi ujitoe kwa dhati.Kubali hata kupoteza utu wako,familia,mume au mke kwa ajili ya Yesu.
-pia ni lazima ukubali kujikana na kubeba msalaba(Mathayo16:24-27).msalaba ni mateso lakini ndiyo ushindi wetu,msalaba ni aibu,kubali aibu kwa ajili ya Kristo.Kubali kunenwa kuwa umechanganyikiwa,kuacha starehe,anasa,dhambi zote hata kama zinavutia kwa ajili ya kristo.unaweza ukaona wenzako kazini wanaiba kwa kuchengesha mahesabu na unaona wanafanikiwa kuwa na nyumba nzuri,magari n.k.wewe usifuatishe acha,jikane,huko ndiko kubeba msalaba.
-Naomba nikukumbushe tenzi za Rohoni wimbo usemao" Bwana u sehemu yangu "kuna mahali mtunzi ameandika"mahali hapa sikutaka niheshimiwe na yanikute mateso sawa sawa na wewe."na chorus yake inasema pamoja na wewe ukimaanisha ushirika na Yesu katika mateso pia.ILI UWE RAFIKI WA YESU KUBALI KUSHIRIKI MATESO PAMOJA NAYE.

5.Hatua ya tano ni uaminifu.(1Kor 4:1-2),Rafiki wa Yesu anajua siri za Mungu nyingi anatakiwa kuwa mwaminifu sana,neno hili kuna maneno mawili ambayo imani na kamili.ili mtu awe mwaminifu lazima awe na imani kamili au imani iliyojitosheleza(faithfull).Na imani kamili ndiyo inatimizwa na kutii kila amri ya kwenye biblia.Kuna siri nyingi utapewa kama rafiki yake na si zote za kusema kwa wakati huo,nyingine unaweza kuambiwa uombe wewe mwenyewe,na nyingine utekeleze kwa matendo,nyingine anaweza kukwambia kama rafiki yake mpendwa lakini hazina utekelezaji japo kakushirikisha,zipo katika mapenzi yake hauwezi badilisha.(Zaburi25:14)

Mfano:
Mungu anaweza kukuambia habari ya mtu kuwa atamchukua au kifo kitampata.hapo pana mambo ya kuzingatia.Je Mungu ameruhusu au ni roho ya mauti.kama roho ya mauti unaweza kukemea lakini kama ni mapenzi yake unapaswa kushukuru.lakini pia inaweza ikawa mapenzi yake lakini ukamsihi asimchukue kwa kupeleka hoja zenye nguvu kwake na kumsihi kama ombi lakini si amri.Yesu aliomba baba ikiwezekana kikombe kiniepuke.sehemu hiyo akutumia mamlaka sababu ni sehemu ambayo ilikuwa katika mamlaka ya Mungu.ni lazima uelewe maombi ya kusihi mapenzi ya Mungu na sehemu ya kutumia mamlaka.Sisi tumepewa kumtii Kristo pia tumepewa kumpinga shetani(Yakobo 4:7)Tukiomba vibaya bila kuelewa hatupati majibu.Mtu anayefikia hatua ya kuwa mwaminifu ataambiwa siri na Mungu hata za mambo yanayotokea mbele kama misiba,baraka,njaa,vita n,k,mengine ni ya kusema na mengine si ya kusema inategemea na maongozi ya Roho Mtakatifu.Mtu mropokaji sana ,asiyetulia,hawezi kupewa siri nyingi.anatafutwa MWAMINIFU ndiye anastahili kuambiwa mambo ya Bwana na atasema kwa maongozi ya Roho tu.Utulivu wa Yohana ulimsaidia kuandika kitabu cha ufunuo chenye siri kubwa juu ya siku za mwisho.Mungu alimteua Musa kuongea naye na kisha kupeleka maagizo kwa Israel.Musa alijua siri za Mungu kutokana na uaminifu wake.maono mengine Mungu anaweza kukupa lakini si ya sasa,ukikurupuka kusema yanaweza kukuletea matatizo.Manabii walipewa mambo ya miaka mingi ijayo na mpaka wanakufa hawakuyaona.wengine wakiambiwa upenda kusema haraka ili wajikweze kuwa wenyewe ni manabii wa kweli.Watu kama hao ni rahisi kushuswa au kutopewa tena.

Mungu awabariki somo litaendelea ili kuzifahamu faida za kuwa rafiki wa Yesu.

Video ya somo hili:https://www.youtube.com/watch?v=qoBJ4EJZmMU

Mchungaji:Lugano Mwakisole


EAGT Paradise Mbagala Zakhem

Sunday, August 31, 2014

Ibada ya Leo Jumapili EAGT Paradise Church

Ibada ya Leo Jumapili EAGT Paradise Church

by Eagt Paradise



August 31, 2014 at 09:43PM

from Facebook

via IFTTTfrom Facebook

via IFTTT

Ni Siku njema ambayo Bwana ametupa,baada ya Siku Sita za kufanya kazi Leo itenge iwe Siku ya kumfanyia Bwana Ibada.

Ni Siku njema ambayo Bwana ametupa,baada ya Siku Sita za kufanya kazi Leo itenge iwe Siku ya kumfanyia Bwana Ibada.

by Eagt Paradise



August 31, 2014 at 10:06AM

from Facebook

via IFTTTfrom Facebook

via IFTTT

Wednesday, August 27, 2014

KUWA RAFIKI WA KARIBU WA YESU-Mch.Lugano Mwakisole

MCHUNGAJI LUGANO MWAKISOLE

KUWA RAFIKI WA KARIBU WA YESU
Kuna utofauti mkubwa kuwa rafiki na mwanafunzi,
Kuwa rafiki wa Yesu ni zaidi ya kuwa mwanafunzi wake,Ni kiwango ambacho si rahisi kwa mwamini kufikia kuwa rafiki wa Karibu wa Yesu,Ni hatua ya juu sana
Ukiwa rafiki wa Yesu unapata nafasi ya kuongaea na nae ana kwa ana,
Katika Somo hili tutajifunza Jinsi Gani sisi kama wanafunzi wa Yesu tunaweza kuwa Rafiki zake wa karibu.Fuata nami na Mungu atakubariki

HATUA ZA KUWA RAFIKI WA YESU.
1.UTII
hatua hii ni ya muhimu sana ili ufikie kuwa rafiki.Yesu amesema ninyi mmekuwa rafiki zangu mkitenda niwaamuruyo(Yohana 15:14),Yesu anathibitisha kuwa ili tuwe marafiki zake ni lazima tutii maagizo yake..kipimo cha  kumpenda Yesu ni kutii maagizo yake.pia katika Yohana 14:21 inasema "Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika,yeye ndiye anipendaye;naye anipendaye atapendwa na Baba yangu,nami nitampenda na kujidhihirisha kwake" mtu anayeshika amri au maagizo ya Yesu ndiye ependwaye na Yesu au anakuwa rafiki wa Yesu.Yesu alimuuliza Petro mara tatu kama kweli anampenda.(Yohana 21:15-17),Petro alipojitetea kwa sababu nyingi na kutaka kuonyesha kuwa anampenda Yesu alimjibu kuwa achunge na kulisha kundi.Kumbuka alimuuliza maswali haya baada ya kufufuka akisikitishwa na Petro kuacha kutii wito aliomwachia kabla ya kufa  na malezi yote aliyompa kwa muda wote aliokaa naye.pia alipomwita aliwambia aache kuvua samaki naye atamfanya kuwa mvuvi wa watu.Muda mfupi tu Yesu alipomwacha ameacha kutii agizo ameenda kuvua samaki.kitendo cha kutokutii wito Yesu akahuzunika sana na kumuuliza kweli anampenda? Tatizo ni kutokutii ndicho Yesu kilichomsononesha.Pia lazima tujiulize mbona anaulizwa Petro si wanafunzi wengine?wakati kwenye kuvua samaki walikuwa wengi,Jibu ni hili Yesu hakutegemea rafiki yake mpendwa au mwanafunzi wa karibu zaidi ndio kaharibu.Ukiwa rafiki wa Yesu ni lazima uwe na utii wa hali ya juu katika maagizo ndipo Yesu atakuwa na imani  nawe.usifanye kitu kitakachosababisha Yesu kuwa na mashaka na urafiki wenu kama Petro.Mimi na wewe tujiulize je tumesimamia wito wetu na kutii kila agizo ili  Yesu atupende kama rafiki zake?

2.KUPENDA KUJIFUNZA
Hii ni hatua ya muhimu na Yesu anaizingatia sana kwa marafiki zake.(Yohana 8:31) Yesu anasema “ninyi mkishika neno langu mmekuwa wanafunzi wangu kwelikweli” kuwa mwanafunzi kwelikweli kwa maana nyingine ni kuwa mwanafunzi anayepita wanafunzi wengine au kuwa rafiki wa karibu.Tuna mfano wa dada aliyekuwa rafiki sana wa Yesu anaitwa Mariam.alikaa miguuni pa Yesu akijifunza.(luka 10:38-42) Yesu alimpenda na akasema amechagua fungu jema,na kihistoria anaonyesha ni miongoni mwa rafiki wa karibu wa Yesu.Sehemu nyingi zinaonyesha kama kufa kwake,kufufuka kwake,na mpaka anapaa alikuwa karibu naye sana.


3.HATUA YA UTOAJI
Hii ni sadaka ya tofauti na sadaka ya kawaida.sadaka ambayo inamgusa Yesu kwa kiwango cha juu.Sadaka ambayo Yesu akiangalia inamkumbusha sadaka yake kubwa aliyoitoa msalabani.ukitoa sadaka ya namna hiyo ni lazima Yesu awe rafiki yako.sadaka hiyo inakufanya wewe uchukuliwe uwe karibu na sadaka ya msalaba.Watu wengi waliotoa kwa kiwango cha juu kama hicho waliugusa moyo wa Yesu na kuwa marafiki zake.
-Mfano wa kwanza ni baba wa imani Ibrahim alikubali kumtoa mwanawe wa pekee  Isaka kuwa sadaka ya kuteketezwa.kitendo cha kutoa mtoto wa pekee ,mpendwa,kilimkumbusha Mungu kumtoa mwanawe wa pekee Yesu kufa msalabani. Unaweza kusema mbona wakati huo Yesu alikuwa bado hajafa.kumbuka mpango wa Yesu kufa ulipangwa na Mungu zamani sana biblia inasema kabla ya kuwekwa misingi ya dunia(1petro1:19-20) kwahiyo utoaji wa Ibrahim ulikuwa utabiri wa Yesu na ulimfanya Ibrahim kumkumbusha Mungu sadaka yake.habari yote unaipata katika kitabu cha mwanzo 22.sura yote.Pia tunaona katika msitari wa 11-12 malaika wa Bwana anamsifia Ibrahim kwa moyo wake wa kumcha Bwana.Mungu aliuona moyo wa Ibrahim baada ya kutoa sadaka ya tofauti.urafiki wa MUNGU na Ibrahim uliongezeka.
 Mstari wa 13 Mungu anatoa kondoo badala ya Isaka,hapa inafundisha kuwa yeyote atakayetoa kwa kiwango cha juu na sadaka ya pekee,maalumu au inayogusa moyo wake Mungu lazima atoe mbadala kwa lugha nyingine Mungu atakulipa kwa njia tofauti kama Ibrahim alivyolipwa
(mst 15-18)

-Mfano mwingine ni Mariam Magdalena.pamoja na kukaa miguuni pa Yesu na kujifunza lakini pia alimtegemeza Yesu kwa mali zake.kuna sadaka moja ilimgusa Yesu,alipompaka Yesu kwa mafuta ya thamani.katika desturi ya wayahud kulikuwa na kutawadha miguu na hii ilikuwa kwa mtumwa kutawadha Bwana wake.Mariam hakutumia kitambaa,yeye  akatumia nywele za kichwa chake,pia wengine walitumia maji lakini yeye alitumia machozi yake na mafuta ya thamani.(Yohana 12:3 na luka7:36-38)kitendo hiki kiligusa moyo wa Yesu na kilimshangaza,mafuta thamani kubwa kumtawadha Yesu,ni sadaka kubwa sana alitoa.Unyenyekevu wa Mariam(kudondosha machozi ishara ya maombi na kumfuta kwa nywele zake kuonyesha kushuka),sadaka yake kubwa(kitendo cha kutojari mali zake kwaajili ya Yesu)na kupenda kukaa miguuni pa Yesu na kujifunza kilifanya Yesu awe rafiki yake zaidi ya wanafunzi wengine.

Bado kuna hatua nyingine tatu ili kukamilisha kuwa rafiki wa Yesu,tutaendelea nazo wiki ijayo siku kama hii.Ombi langu tafuta kuwa rafiki wa Yesu utapata faida nyingi ambazo utazifahamu utakapoendelea na somo mpaka mwisho.
MUNGU AWABARIKI.


Mchungaji:Lugano Mwakisole

EAGT Paradise Mbagala Zakhem