Tuesday, October 22, 2013

YALIYOJIRI KATIKA IBADA YA JUMAPILI 20.10.2013 KATIKA PICHA


KIPINGI CHA SIFA

Mtumishi wa Mungu Reuben akiongoza kipindi cha Sifa
Kumtumikia Mungu hakuna mipaka ni mtumishi wa Mungu kutoka Arusha

Kwa Yesu Kunalipa


Mtumishi wa Mungu kutoka mito ya Baraka alikuwepo kumsifu Mungu
Ilifika zamu ya Kwaya ya Kanisa la Paradise kumsifu na kumwimbia Mungu

Mtumishi wa Mungu Mwimbaji binafsi kutoka kanisa la Paradise Mchopa akimwimbia Mungu





Kwaya ya wamama wa Paradise nayo haikuwa nyuma kumwimbia Mungu




WAKATI WA MAHUBIRI YA NENO LA MUNGU

Mtumishi wa Mungu Mchungaji Lugano Akihubiri Neno la Mungu





WAKATI WA MAOMBI NA MAOMBEZI

Baadhi ya washirika wa EAGT Paradise wakiwa kwenye Maombi




Mtumishi wa Mungu Joseph akitenda kazi









Monday, October 21, 2013

IBADA YA JUMAMOSI 19.10.2013 KATIKA PICHA

Katika siku ya Jumamosi tar 19.10.2013,kulifanyika ibada ya kumtukuza Mungu katika kanisa la EAGT Paradise.

Ibada hiyo ilikuwa ni maalum kwa ajili ya maombi ya UAMSHO WA KANISA LA MUNGU.

Nguvu za Mungu zilitembea sana na walihudhuria walishuhudia kuwa kweli wamekutana na nguvu za Mungu.

Tunakuletea matukio katika picha.

Maandalizi ya kipindi cha sifa
Mtumishi wa Mungu Reuben akiongoza kipindi cha sifa


Mchungaji kiongozi wa Kanisa la EAGT Paradise akihubiri katika ibada hiyo
Neno la Mungu ni nguzo katika kila kitu Mchungaji Lugano akisoma maneno ya Mungu kutoka katika Biblia Takatifu







Thursday, August 29, 2013

BREAKING NEWS: ASKOFU MOSES KULOLA AFARIKI DUNIA




Taarifa zimeenea  hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia muda mfupi uluopita.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika ambazo tumezipata kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.

Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.

Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.



Gospel Kitaa itaendelea kukufahamisha kwa kadri ambavyo taarifa zitakuwa zikitufikia.Kufahamu historia ya maisha ya Hayati Askofu Dr. Moses Kulola .

BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe.


Source:Gospel Kitaa

Monday, August 26, 2013

ANGALIA PICHA ZA MKUTANO WA REINARD BONNKE VIWANJA VYA TAIFA

Angalia baadhi ya picha za mkutano mkubwa wa injili ulioandaliwa na huduma ya mwinjilisti wa kimataifa Reinhard Bonnke akiwakilishwa na kijana wake katika huduma Daniel Kolenda, mkutano ambao unafanyika katika uwanja wa nje wa taifa jijini Dar es salaam. ukishirikisha watumishi kutoka makanisa mbalimbali.